Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 16, 2024 Local time: 03:32

Afisa katika UN anaahidi viwango vya ajira kwa wahamiaji vinaheshimiwa Saudia.


Bendera ya Saudi Arabia
Bendera ya Saudi Arabia

Siku mbili kabla ya FIFA kuithibitisha Saudi Arabia kuwa mwenyeji wa Kombe la Dunia 2034 afisa wa ngazi ya juu wa haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa aliahidi Jumatatu kujaribu kuhakikisha viwango vya ajira kwa wahamiaji vinaheshimiwa sana wakati wa mashindano hayo.

Saudi Arabia ni mgombea pekee na ana uhakika wa kushinda siku ya Jumatano wakati FIFA itakapofanya mkutano kwa njia ya mtandao wa mashirikisho yake ya wanachama wa 211 ili kutoa haki za mwenyeji wa 2034 kwa kuthibitisha bila kura ya maoni.

Mpango wa Kombe la Dunia kwenye ufalme wenye utajiri wa mafuta unahitaji kujenga viwanja nane kati ya 15 vilivyoahidiwa kutoka mwanzo, pamoja na kuongeza vyumba vya hoteli 175,000. Itategemea sana wafanyakazi wahamiaji, mara nyingi kutoka Asia Kusini ndani ya mfumo wa sheria ya kazi ambapo makundi ya wanaharakati yanasema sheria haziwalindi.

Siku ya Jumatatu, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk, alisema shirika lake huko Geneva halihusiki moja kwa moja na FIFA juu ya masuala ya Kombe la Dunia.

Forum

XS
SM
MD
LG