Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Januari 21, 2025 Local time: 13:02

Watu 28 wauawa katika shambulizi la kombora kwenye kituo cha mafuta mjini Khartoum


Picha hii inaonyesha nyumba iliyoshambuliwa mjini Khartoum katika mapigano kati ya jeshi la serikali na kikosi cha Rapid Support Forces( RSF), Aprili 25, 2023. Picha ya AP
Picha hii inaonyesha nyumba iliyoshambuliwa mjini Khartoum katika mapigano kati ya jeshi la serikali na kikosi cha Rapid Support Forces( RSF), Aprili 25, 2023. Picha ya AP

Mtandao wa kundi la waokoaji wa kujitolea nchini Sudan umesema raia 28 wameuawa Jumapili wakati kituo cha mafuta kilichopo katika eneo la Khartoum chini ya udhibiti wa kundi la RSF kiliposhambuliwa kwa makombora.

Jeshi la Sudan, ambalo limekuwa likipigana na kikosi cha Rapid Support Forces (RSF) tangu Aprili 2023, Limeweza kusonga mbele kuelekea mji mkuu katika wiki za hivi karibuni, kwa lengo la kuudhibiti tena mji wa Khartoum.

Jumapili, kituo cha mafuta katika eneo la kusini mwa Khartoum linalodhibitiwa na RSF kilishambuliwa kwa makombora, limesema kundi la The South Belt Emergency Response Room.

Kundi hilo la kujitolea linaloongozwa na vijana limesema “watu 28 wamethibitishwa kufariki” na idadi ya waliojeruhuwa imefikia 37, ikiwa ni pamoja na 29 walioungua moto” na baadhi wana majeraha mabaya.

Forum

XS
SM
MD
LG