Ugonjwa usiojulikana huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo umesambaa zaidi miongoni mwa watoto na kuwaweka watu kwenye hatari ya kupata utapiamlo uliokithiri, kulingana na
Shirika la Afya Duniani (WHO) ambalo limepeleka wataalam wake katika eneo hilo kuchunguza mlipuko huo. Katika taarifa mpya iliyochapishwa Jumapili, WHO ilisema kesi 406 za ugonjwa huo usiojulikana zilirekodiwa kati ya Oktoba 24 hadi
Disemba 5, ambapo wagonjwa 31 walifariki. Dalili za ugonjwa huo, na chanzo chake hakijaelezwa, inajumuisha homa, maumivu ya kichwa, kikohozi, mafua na maumivu ya mwili. Umeenea katika kituo cha afya cha Panzi huko kusini-magharibi mwa jimbo la Kwango nchini DRC.
Kesi zote ziliripotiwa kuwa na utapiamlo mkali, na idadi kubwa ya kesi hizo zilizoripotiwa ni watoto, hasa wenye umri chini ya miaka mitano, WHO imesema.
Forum