Mapinduzi yametokea baada ya mashambulio yaliyofanyika kwa kasi yaliyoanzishwa na muungano wa makundi ya upinzani karibu siku 10 zilizopita kutoka mji wa Idlib, kaskazini mashariki mwa Syria.
Mkuu wa kundi lililokua linafuatilia vita vya Syria, Rami Abdel Rahman anasema, Rais Bashar al-Assad ameondoka kuelekea mahala kusikojulikana nje ya nchi.
Inasemekana alikimbia kabla ya waasi kusema wameingia Damascus baada ya kuteka miji mingine ya nchi katika tukio la kipekee kwa haraka.
Waziri mkuu wa Syria, Mohammed Ghazi al-Jalali amesema serikali yake iko tayari kufanya kazi na upinzani na kukabidhi madaraka kwa serikali ya mpito itakayo chaguliwa na wananchi wa Syria.
Katika ujumbe wa ideo kwenye ukurasa wake wa Facebook, Jalali, amesema "niko nyumbani kwangu, sijaondoka kwa sababu hii ni nchi yangu pia."
Amesema atakwenda ofisini asubuhi kuendelea na kazi na yuko tayari kushirikiana na upinzani na kutoa wito kwa wananchi wa Syria kutoharibu mali za umma.
Hakuna taarifa rasmi iliyotolewa na serikali juu ya matukio haya ambayo hayakutarajiwa.
Kiongozi wa kundi la waasi la Hayat Tahrir al-Sham (HTS) Abu Mohammed Al-Golani amewataka wapiganaji wake kutoharibu mali za serikali, akiwataka wasiwashambulie wanajeshi wanaojisalimisha au kuwafuata wanaokimbia.
Wachambuzi wanasema matukio hayo yote ni ishara nzuri ya ushirikiano kati ya upinzani na wakuu wa serikali kuweza kushirikiana kupanga mustakbal mpya kwa Syria.
Forum