Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 04:56

Trump aahidi kufanya marekebisho makubwa baada ya kuingia ofisi Januari 20


Rais mteule wa Marekani Donald Trump.
Rais mteule wa Marekani Donald Trump.

Rais-mteule wa Marekani, Donald Trump ameapa kufanya  mabadiliko makubwa na ya haraka baada ya kuchukua ofisi Januari 20, kwa kuwarudisha makwao mamilioni ya wahamiaji walio ndani ya nchi kinyume cha sheria.

Pia ameahidi kupandisha ushuru kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka nje, hali ambayo inaweza kusababisha kupanda bei kwa bidhaa kwa wamarekani, pamoja na kutoa msamaha kwa waandamanaji ambao walijaribu kubadili matokeo ya ya uchaguzi wa 2020 ambao alishindwa.

Ikiwa zimebaki wiki 6 kabla ya kuchukua madaraka kwa muhula mpya wa miaka 4 katika White House, Trump anaonekana amepata ujasiri kutoka na ushindi wake mwezi uliopita akiwa rais wa pili wa Marekani kuchaguliwa kwa muhula wa pili usiofatana sawa na rais Grover Cleveland katika miaka 1890.

Katika mahojiano na kituo cha televishenio cha NBC katika kipindi cha Meet the Press mwishoni mwa wiki, Trump alisema kuwa, “ muhula huu utakuwa tofauti, niliposhinda kwa mara ya kwanza 2016 sikuwa na umaarufu mkubwa kama ilivyo sasa.” “Kilicho muhimu sana wakati huu ni kwamba nilishinda kwa kura nyingi takriban milioni 2.3 mbele ya mshindani wangu Kamala Harris kati ya jumla ya kura milioni 155 zilizopigwa.

Forum

XS
SM
MD
LG