Taarifa imesema hatua hiyo inafuatia mkutano kati ya viongozi wa makundi yenye silaha na kiongozi wa mpito Ahmad al-Sharaa, aliyeongoza waasi waliomuondoa madarakani kiongozi wa muda mrefu Bashar al-Assad.
Waasi walidhibithi mku mkuuu wa Damascus Desemba 8, baada ya kudhibithi miji mingine ya Syria baada ya miaka 13 ya mapigano na kupelekea utawala wa Assad kuanguka.
Tangu Assad kuondoka madarakani, serikali kadhaa katika kanda hiyo ya mashariki ya kati zimetuma wajumbe mjini Damascus kujadilia hali ya baadaye ya Syria na utulivu wa kanda hiyo.
Kati ya maswala yanayozungumziwa zaidi ni uwezekano wa kurudi tena kwa kundi la Islamic state, ambalo lilidhibithi sehemu za mashariki mwa Syria hapo mwaka 2014, na magharibi mwa Iraq kabla ya kupoteza udhibithi wake.
Forum