Serikali ya Uturuki inatambua kundi la YPG kuwa sehemu ya chama cha kikurdi cha PKK, ambalo ni kundi la wapiganaji ambalo limekuwa likipigana na Uturuki kwa miaka 40. Wanachukuliwa kuwa kundi la kigaidi na Ankara, Washington na umoja wa ulaya.
Erdogan amesema Ankara imeendelea kuwa na ushirikiano wa karibu na kiongozi wa mpito wa Syria Ahmed al-Sharaa, na kwamba maafisa wa Uturuki wataendeela kutembelea Syria.
Hii ni baada ya Waziri wa mambo ya nje wa Ankara Hakan Fidan kufanya mazungumzo na maafisa wa Syria mjini Damascus.
Forum