Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 21, 2024 Local time: 20:07

Marekani: Mswada wa bajeti unaoungwa mkono na Trump umefeli


Spika wa baraza la Congress Mike Johnson (Kulia) baada ya kikao na waandishi wa habari Septemba 24 2024
Spika wa baraza la Congress Mike Johnson (Kulia) baada ya kikao na waandishi wa habari Septemba 24 2024

Mswada wa kufadhili bajeti ya serikali kuu unaoungwa mkono na rais mteule Donald Trump, umeshindwa kupitishwa na baraza la wawakilishi.

Darzeni ya warepublican walikataa kufuata maagizo ya rais mteule Donald Trump, kutaka mswada huo upitishwe jana alhamisi.

Hatua hiyo imepelekea baraza la wawakilishi kukosa mwelekeo namna ya kuzuia serikali kuu kufungwa, hatua inayoweza kuvuruga mipangilio ya sherehe za krisimasi kwa wamarekani.

Kukosa kupitishwa mswada wa bajeti, ni hatua inayoweka taaswira namna chama cha Republican kinaweza kuwa na wakati mgumu katika uatawala wake kuanzia mwaka ujao, Trump atakapoingia madarakani.

Chama cha Republican kinadhibithi baraza la wawakilishi na senate.

Baraza la wawakilishi limekataa mswada wenye lengo la kuongeza matumizi ya fedha za serikali na kuruhusu mpango ambao unaongeza trilioni za dola kwa serikali kuu, na kuongeza deni la dola trilioni 36

Forum

XS
SM
MD
LG