Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 21, 2024 Local time: 20:19

Wanadiplomasia wa Marekani wamewasili Syria


muonekano wa mji mkuu wa Syria, Damascus. Desemba 20, 2024
muonekano wa mji mkuu wa Syria, Damascus. Desemba 20, 2024

Wanadiplomasia wa ngazi ya juu wa Marekani kutoka utawala wa Joe Biden wako Damascus, Syria kwa mkutano na maafisa wa utawala wa Syria wakiongozwa na Hayat Tahrir al-Sham.

Hayo ni kulingana na wizara ya mambo ya nje ya Marekani.

Mkutano huo ni wa kwanza wa ana kwa ana kati ya maafisa wa Washington na viongozi wa muda wa Syria.

Mwanadiplomasia wa ngazi ya juu wa Marekani kuhusu maswala ya mashariki ya kati, Barbara Leaf, mjumbe wa rais kuhusu utekaji nyara Roger Carstens na mshauri wa ngazi ya juu Daniel Rubinstein, ambaye anaongoza ofisi inayohusika na maswala ya Syria, ni wanadiplomasia wa kwanza wa Marekani kuzuru Damascus tangu waasi kuuangusha utawala wa rais Bashar al-Assad.

Ziara yao inajiri wakati serikali za magharibi zinafungua njia za kushirikiana na uongozi mpya wa Syria na kiongozi wake Ahmed al-Sharaa na kuanza majadiliano iwapo kundi hilo linastahili kuondolewa kwenye orodha ya magaidi.

Forum

XS
SM
MD
LG