Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Januari 21, 2025 Local time: 12:55

Majanga yamesababisha hasara ya dola bilioni 310 mwaka 2024


Picha hii inaonyesha mwoto katika Kaunti ya Tehama, California, Agosti 7, 2024. Picha ya AP
Picha hii inaonyesha mwoto katika Kaunti ya Tehama, California, Agosti 7, 2024. Picha ya AP

Kampuni kubwa ya bima yenye makao yake Uswizi Alhamisi imesema majanga kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa yamesababisha hasara ya kiuchumi ya dola bilioni 310 ulimwenguni mwaka 2024.

Mwaka wa 2024 ulikuwa wenye joto kali kuwahi kushuhudiwa.

Hasara ya kiuchumi kutokana na majanga inakadiriwa kuongezeka kwa asilimia 6 ikilinganishwa na mwaka 2023, kampuni ya Swiss Re imesema katika taarifa.

Kwa jumla, hasara ya bima iliongezeka kwa asilimia 17 kwa mwaka hadi dola bilioni 135, huku vimbunga vya Helene na Milton nchini Marekani na mafuriko makubwa barani Ulaya yakizidisha hasara, kampuni hiyo imesema.

Ni kwa mara ya tano mfululizo hasara ya bima ikifikia dola bilioni 100, kampuni hiyo ya Uswizi imesema.

Forum

XS
SM
MD
LG