Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 04:09

Marekani yaendelea kujadili udukuzi wa China


Bunge la Marekani, mjini Washington DC
Bunge la Marekani, mjini Washington DC

Idara za serekali ya Marekani, zilifanya mkutano wa siri na Maseneta Jumatano, kuhusu udukuzi wa China ambao unajulikana kama “Salt Typhoon,” uliojikita ndani kabisa mwa mashirika ya mawasiliano ya simu ya Marekani, na kuiba taarifa za simu za Marekani.

FBI, Mkurugenzi wa Idara ya taifa ya Ujasusi, Avri Haines, Mwenyekiti wa tume ya taifa ya mawasiliano, Jessica Rosenworcel, Baraza la usalama wa taifa, na Idara ya ulinzi wa miundombinu ya mtandao walikuwa miongoni mwa washiriki wa mkutano huo wa faragha kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters.

Seneta wa chama cha Demokrat, Ron Wayden, amewaambia wanahabari baada ya kikao kwamba alikuwa akifanyia kazi rasimu ya muswada wa jambo hilo, huku Seneta Bob Casey, akisema ana wasiwasi mkubwa kuhusu shauri hilo na kuongeza kwamba inaweza isifanikiwe mpaka mwakani kwa bunge kushughulikia tatizo hilo.

Forum

XS
SM
MD
LG