Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 12, 2025 Local time: 23:07

UM watahadharisha hali ya Syria


Mjumbe wa Umoja wa Mataifa kwa Syria, Jumanne ameonya vita bado havijakwisha, nchi hiyo ni tete na inakabiliwa na changamoto nyingi, lazima iende kwa kasi kuelekea kipindi cha mpito wa kisiasa kinacho jumuisha pande zote.

“Kuna matumaini makubwa kwamba Syria sasa ina nafasi ya kweli ya kuelekea kwenye amani, utulivu wa kiuchumi na ukuaji, ushirikishwaji wa Wasyria wote na uwajibikaji na haki,” Geir Pedersen ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Ameongeza kusema kwamba bado wengi wana wasiwasi kuhusu mustakabali wa nchi. Ametaja changamoto zilizo mbele kuwa ni kubwa, na wasiwasi ni kwamba, kama hili halitashughulikiwa ipasavyo na Wasyria na jumuiya ya kimataifa, basi kuna uwezekano wa hali kugeuka na kuwa mbaya zaidi.

Alizungumza akiwa Damascus, ambapo alikutana na kamanda wa utawala mpya, Ahmed al-Sharaa, na waziri mkuu wa serekali ya muda, Mohammed al-Bashir.

Forum

XS
SM
MD
LG