Luigi Mangione tayari ameshtakiwa kwa mauaji ya Desemba 4 ya Brian Thompson, lakini mashitaka ya ugaidi ni mapya.
Chini ya sheria ya New York, mashitaka kama hayo yanaweza kuletwa wakati uhalifu unakusudiwa kuwatisha au kuwalazimisha raia, kushawishi sera za kitengo cha serikali kwa vitisho au kulazimishwa na kuathiri mwenendo wa kitengo cha serikali kwa mauaji au utekaji.
Wakili wa Mangione, wa New York hajazungumzia mashitaka hayo. Thompson, 50, alipigwa risasi na kufa alipokuwa akitembea kuelekea hoteli ya Manhattan ambako UnitedHealthcare yenye makao yake Minnesota, bima kubwa ya matibabu Marekani, ilikuwa ikifanya mkutano wa wawekezaji.
Forum