Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 21, 2024 Local time: 21:23

Idadi ya vifo kutokana na kimbunga Chido nchini Msumbiji yafikia 45


Picha hii inaonyesha uharibifu uliosababishwa na kimbunga Chido nchini Msumbiji
Picha hii inaonyesha uharibifu uliosababishwa na kimbunga Chido nchini Msumbiji

Idadi ya vifo kutokana na kimbunga Chido nchini Msumbiji imeongezeka kutoka 11 hadi 45, idara ya taifa ya usimamizi wa majanga imesema Jumatano.

Takwim zilizotolewa Jumanne zilisema kimbunga kimeua watu 34 baada ya kufika nchini Msumbiji siku ya Jumapili katika jimbo la kaskazini la Cabo Delgado.

Idara hiyo imesema watu 38 walifariki huko Cabo Delgado, wanne katika mkoa wa Nampula na watatu huko Niassa, na mtu mwingine alitoweka.

Watu 500 wameripotiwa kujeruhiwa na kimbunga hicho, ambacho kimesababisha upepo wa kasi ya kilomita 260 kwa saa na mvua kubwa sana katika saa 24, idara hiyo imesema.

Takriban nyumba 24,000 ziliharibika na nyingine 12,300 kuharibika kidogo, idara hiyo imesema. Zaidi ya watu 181,000 wameathiriwa na kimbunga hicho.

Forum

XS
SM
MD
LG