“Wanajeshi wa Korea Kaskazini wamehusika katika mapigano katika mkoa wa Kursk wakiwa pamoja na vikosi vya Russia,” msemaji wa Pentagon, Meja Jenerali Pat Ryder aliwaambia waandishi wa habari Jumatatu.
Amesema wamekuwa wakipoteza maisha na kujeruhiwa, akiongeza kuwa ushiriki wa wanajeshi wa Korea Kaskazini katika vita kwa sasa ni mdogo kwa Kursk, ambao ni mkoa wa Russia.
Pentagon haikueleza zaidi juu ya kiwango cha maafa kwa Korea Kaskazini.
VOA iliwasiliana na ubalozi wa Russia, Washington, lakini haikujibu maombi ya kutoa ufafanuzi wa shauri hili.
Msemaji wa Kremlin, alielekeza maswali kuhusu tathmini ya Marekani kwa Wizara ya Ulinzi ya Russia, ambayo pia bado haijatoa maoni.
Forum