Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Januari 21, 2025 Local time: 12:47

Viongozi wa ECOWAS wakutana kujadili usalama katika kanda ya Sahel


Rais wa Senegal Basirou Diomaye Faye akihuduria mkutano wa ECOWAS mjini Abuja, Julai 7.2024. Picha ya AP
Rais wa Senegal Basirou Diomaye Faye akihuduria mkutano wa ECOWAS mjini Abuja, Julai 7.2024. Picha ya AP

Viongozi kutoka nchi wanachama wa Jumuia ya Uchumi ya Afrika Magharibi ECOWAS walikutana Jumapili katika mkutano kuhusu usalama na kuondoka kwenye jumuiya hiyo kwa serikali tatu zinazoongozwa na wanajeshi.

Kabla ya mkutano huo wa ECOWAS, Burkina Faso, Mali na Niger zimesisitiza tena kwamba hazitobadili uamuzi wao wa kujiondoa kwenye jumuiya hiyo, zikidai ECOWAS ni kibaraka wa Ufaransa.

Kuondoka kwa nchi hizo tatu kuna athari kubwa kwenye biashara huru na usafiri wa watu pamoja na ushirikiano wa usalama katika kanda hiyo ambapo makundi ya wanajihadi yanazidi kudhibiti maeneo katika kanda ya Sahel.

Miongoni mwa viongozi waliohudhuria mkutano huo katika mji mkuu wa Nigeria, Abuja, ni Rais wa Senegal Bassirou Diomaye Faye, ambaye aliteuliwa kama mpatanishi na ECOWAS mwezi Julai.

Faye alisema wiki iliyopita kwamba alipiga hatua katika mazungumzo na nchi hizo tatu na kusema hakuna sababu kwa nchi hizo kutoshirikiana na nchi wanachama wengine, hasa kutokana na hali ya usalama.

Forum

XS
SM
MD
LG