Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Januari 21, 2025 Local time: 13:54

Israel inasema Syria bado ni tishio kwa usalama wake


Waziri mpya wa ulinzi wa Israel, Israel Katz
Waziri mpya wa ulinzi wa Israel, Israel Katz

Vitisho dhidi ya Israel kutoka Syria bado vipo licha ya kauli za msimamo wa wastani za viongozi wa waasi waliomuondoa madarakani Rais Bashar al-Assad wiki moja iliyopita, waziri wa ulinzi wa Israel Katz alisema Jumapili, huku kukiwa na harakati za kijeshi za nchi yake kukabiliana na vitisho hivyo.

“Hatari za mara moja kwa nchi yetu bado zipo na matukio ya hivi karibuni nchini Syria yanaongeza kasi ya tishio, licha ya taswira ya wastani ambayo viongozi wa waasi wanadai kutoa,” Katz aliwambia maafisa wanaokagua bajeti ya ulinzi ya nchi hiyo, kulingana na taarifa.

Kiongozi wa Syria aliyechukuwa madaraka, Ahmad al-Sharaa alisema Jumamosi kwamba Israel inatumia visingizio vya uongo kuhalalisha mashambulizi yake dhidi ya Syria, lakini amesema hana nia ya kuingia katika mizozo mipya akisema lengo kwa sasa ni kukarabati nchi.

Israel, ambayo ilisema haina nia ya kubaki Syria imetaja kupeleka majeshi yake ndani ya Syria ni hatua ya muda ili kuhakikisha usalama kwenye mpaka, ilifanya pia mamia ya mashambulizi kwenye maghala ya silaha ya Syria.

Forum

XS
SM
MD
LG