Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 13, 2025 Local time: 00:59

Qatar kufungua ubalozi wake Syria


Lango la kuingilia ubalozi wa Qatar, mjini Damascus, Desemba 12, 2024.
Lango la kuingilia ubalozi wa Qatar, mjini Damascus, Desemba 12, 2024.

Ubalozi wa Qatar, nchini Syria, utaanza tena shughuli zake Jumanne, ufalme wa Ghuba ulitangaza Jumapili wakati wanadiplomasia wake walipoitembelea nchi hiyo na kukutana na serikali yake ya mpito kufuatia kuondolewa madarakani kwa Rais Bashar al-Assad.

“Qatar inatangaza kurejesha kazi zake za ubalozi katika Jamhuri ya Kiarabu ya Syria kuanzia kesho Jumanne,” wizara ya mambo ya nje imesema katika taarifa.

Pia ilimtaja mkuu mpya wa ubalozi wa Syria, Khalifa Abdullah Al Mahmoud Al-Sharif.

Doha ilifunga ubalozi wake mjini Damascus na kumrejesha nyumbani balozi wake Julai 2011, katika uasi dhidi ya serikali ya Assad ambao uligeuka kuwa vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Tofauti na nchi nyingine za Kiarabu, Qatar haikuwahi kurejesha uhusiano wa kidiplomasia na Syria chini ya utawala wa Assad, ambaye aliondolewa na harakati za uasi za siku 11 ambazo zilipitia miji mikubwa na kufika mji mkuu Damascus.

Forum

XS
SM
MD
LG