Mahakama ya Katiba ya Korea Kusini leo Jumatatu ilianza kupitia upya mashtaka ya kutaka kumuondoa madarakani Rais Yoon Suk Yeol kwa tangazo lake la sheria ya kijeshi la Disemba 3 na kuanza mchakato wa kuamua kama ataondolewa madarakani, wakati wachunguzi wanapanga kumhoji wiki hii juu ya mashtaka ya uhalifu.
Mahakama hiyo itafanya kikao cha kwanza cha umma hapo Disemba 27, msemaji Lee Jean aliwaambia waandishi wa habari baada ya majaji sita wa mahakama hiyo kukutana ili kujadili mipango ya kutathmini mashtaka ya kumuondoa madarakani, na bunge linalodhibitiwa na upinzani siku ya Jumamosi.
Mahakama hiyo ina hadi miezi sita kuamua iwapo itamuondoa Yoon madarakani au kumrejesha. Usikilizaji wa kwanza utakuwa “maandalizi” ya kuthibitisha masuala makuu ya kisheria ya kesi na ratiba kati ya mambo mengine, Lee alisema.
Forum