Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier leo Ijumaa ameamuru bunge kuvunjwa na kupanga uchaguzi mpya ufanyike Februari 23 kufuatia kuanguka kwa muungano wa utawala wa kansela Olaf Scholz.
Bunge lilipiga kura ya kutokua na imani na Scholz Desemba 16 baada ya serikali ya mseto ya vyama vitatu ambayo haikua mashuhuri kusambaratika Novemba 6 wakati alipomuachisha kazi waziri wake wa fedha kutokana na mvutano juu ya namna ya kufufua Uchumi unaoduma wa Ujerumani.
Viongozi wa vyama kadhaa vikuu walikubaliana kwamba ni lazima uchaguzi wa bunge ufanyike Februari 23 ikiwa ni miezi saba mapema kuliko ilivyopangwa awali. Kwa kuwa katiba ya baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia hairuhusu bunge kujivunja lenyewe, ilikuwa ni jukumu la Steinmeier kuamua kama anavunja bunge na kuitisha uchaguzi.
Steinmeier alikuwa na siku 21 za kuchukua uamuzi huo. Mara baada ya bunge kuvunjwa ni kwamba uchaguzi lazima ufanyike ndani ya siku 60.
Forum