Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 20, 2024 Local time: 14:41

Mazungumzo ya amani kati ya DRC na Rwanda yakwama


Rais Paul Kagame, Rais Joao Lourenco na RaisFelix Tshisekedi, Luanda, Julai 6, 2022. Picha ya AFP
Rais Paul Kagame, Rais Joao Lourenco na RaisFelix Tshisekedi, Luanda, Julai 6, 2022. Picha ya AFP

Mazungumzo kati ya viongozi wa Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ili kumaliza mzozo wa mashariki mwa DRC hayakufanyika tena leo Jumapili kama ilivyotarajiwa kutokana na mivutano kati ya serikali za nchi hizo mbili, maafisa wamesema.

Kundi la waasi wa M23 ambalo linadaiwa kuungwa mkono na Rwanda limeteka maeneo kadhaa mashariki mwa DRC na kusababisha maelfu ya watu kuhama makazi yao na kuchochea mzozo wa kibinadamu.

Kulikuwa na matumaini kwamba mkutano ambao ungesimamiwa na Rais wa Angola Joao Laourenco, mpatanishi aliyeteuliwa na Umoja wa Afrika, ungefikia makubaliano ya kumaliza mzozo wa mashariki mwa Congo.

Lakini Jumapili mchana, mkuu wa ofisi ya mawasiliano kwenye ofisi ya rais wa Angola alisema mazungumzo hayatafanyika.

“Kinyume na kile kilichokuwa kinatarajiwa, mkutano hautafanyika leo,” Mario Jorge amewaambia waandishi wa habari.

Lourenco alikutana na Rais wa DRC Felix Tshisekedi bila kuwepo Rais wa Rwanda Paul Kagame, alisema.

Ofisi ya rais wa Congo ilisema mashauriano yaligonga mwamba baada ya ombi la Rwanda la kutaka DRC kufanya mazungumzo ya moja kwa moja na waasi wa M23.

“Mambo yamekwama kwa sababu Rwanda ilitoa masharti kabla ya kusaini makubaliano ikiiomba DRC kufanya mazungumzo ya moja kwa moja na M23,” Giscard Kusema, msemaji wa ofisi ya rais wa Congo ameiambia AFP, akiwa mjini Luanda.

Forum

XS
SM
MD
LG