Bunge la Korea Kusini limepiga kura kumshtaki kutaka kumuondoa madarakani Rais Yoon Suk Yeol kwa tangazo lake la muda mfupi la sheria ya kijeshi mwezi huu.
Bunge la Taifa lilipitisha hoja hiyo kwa kura 204 kwa 85 leo Jumamosi. Madaraka na majukumu ya urais ya Yoon yatasimamishwa baada ya nakala za hati kuhusu mashtaka kuwasilishwa kwake na kwa Mahakama ya Kikatiba.
Mahakama hiyo ina hadi siku 180 kuamua ikiwa itamfukuza Yoon kama rais au kurejesha mamlaka yake. Iwapo atafukuzwa madarakani uchaguzi wa kitaifa wa kumchagua mrithi wake lazima ufanywe ndani ya siku 60.
Forum