Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 16, 2024 Local time: 03:50

Rais mteule wa Ghana John Dramani Mahama amesema hataachana na  mpango wa IMF


Rais mteule wa Ghana John Dramani Mahama, alipozungumza na Reuters mjini Accra.
Rais mteule wa Ghana John Dramani Mahama, alipozungumza na Reuters mjini Accra.

Rais mteule wa Ghana John Dramani Mahama amesema hataachana na  mpango wa dola bilioni 3 wa kuokoa uchumi wa  nchi hiyo na Shirika la Kimataifa la Fedha -IMF,

Rais mteule wa Ghana John Dramani Mahama amesema hataachana na mpango wa dola bilioni 3 wa kuokoa uchumi wa nchi hiyo na Shirika la Kimataifa la Fedha -IMF, lakini anataka kuutathmini mpango huo ili kukabiliana na matumizi mabaya ya serikali na kuboresha sekta ya nishati

Mahama rais wa zamani ambaye alishinda uchaguzi wa Desemba 7 kwa kura nyingi, aliiambia Reuters Ijumaa jioni pia atajaribu kushughulikia mfumuko wa bei na kushuka kwa thamani ya sarafu ili kupunguza mzozo wa gharama ya maisha katika taifa hilo la Afrika Magharibi.

Mahama alikuwa amesema hapo awali kwamba angejadili upya mpango wa IMF ulioimarishwa na serikali ya Rais anayemaliza muda wake Nana Akufo mnamo mwaka 2023.

Tume ya uchaguzi ya Ghana ilimtangaza Mahama, ambaye alikuwa madarakani kuanzia mwaka 2012-16, mshindi wa urais kwa asilimia 56.55 ya kura.

Rais-mteule katika nchi ambayo ni moja ya mzalishaji nambari mbili wa kakao duniani analirithi taifa kutoka katika mzozo mbaya sana wa uchumi katika kizazi, huku kukiwa na mtikisiko katika sekta yake muhimu ya kakao na dhahabu.

Forum

XS
SM
MD
LG