Mazungumzo ya Umoja wa Mataifa yanayosimamiwa na Saudi Arabia yalishindwa kufikia makubaliano ya jinsi ya kukabiliana na ukame, washiriki walisema leo Jumamosi, wakiwa hawana matumaini ya kuwepo kwa itifaki ya kushughulikia janga hilo linaloongezeka.
Mkutano huo wa siku 12 wa pande zinazohusika katika Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Kupambana na Kuenea kwa Jangwa (UNCCD), unaojulikana kama COP-16, ulihitimishwa mapema leo asubuhi, siku moja baadaye kuliko ilivyopangwa wakati wahusika wakijaribu kufanikisha makubaliano.
Kabla ya mazungumzo hayo, Katibu Mtendaji wa UNCCD Ibrahim Thiaw alisema ulimwengu unatazamia wapatanishi kupitisha uamuzi wa kijasiri ambao unaweza kusaidia kugeuza wimbi la janga lililoenea na linalosumbua zaidi mazingira la ukame.
Forum