Mchezaji soka wa zamani Mikheil Kave-lashvili amechaguliwa kuwa rais wa Georgia huku chama tawala kikizidi kujiimarisha katika kile ambacho upinzani unakiita pigo kwa matarajio ya Umoja wa Ulaya na ushindi kwa Russia.
Kave-lashvili alishinda kwa urahisi upigaji kura wa Jumamosi kutokana na chama cha Georgian Dream kudhibiti viti 300 vya wajumbe ambapo vilibadilisha uchaguzi wa kura za moja kwa moja za rais mwaka wa 2017. Georgian Dream ilichukua tena udhibiti wa Bunge katika uchaguzi wa Oktoba 26 ambao upinzani unadai ulivurugwa kwa msaada wa Moscow.
Rais wa Georgia anayemaliza muda wake na vyama vikuu vinavyounga mkono Magharibi vimelisusia Bunge na kutaka kura irudiwe.
Forum