Kyiv iliwarudisha nyumbani mateka 189, Rais Volodymyr Zelenskyy na Wizara ya Ulinzi ya Russia imesema, wakati wizara ya Russia ikisema wanajeshi 150 wa Russia walirejea nyumbani.
Wizara ya Russia, imesema mateka hao wameachiliwa Belarus, mshirika wa karibu wa Moscow katika vita vilivyodumu kwa miezi 34 na Ukraine, na watahamishiwa Russia.
Picha za televisheni za Reuters nchini Ukraine zilionyesha wenza wa baadhi ya watumishi waliokuwa wakiwangoja, wengi wao wakiwa wamevalishwa bendera za taifa wakilia walipounganishwa tena baada ya giza kuingia nje ya jengo.
Forum