Yoon anakabiliwa na mashtaka ya kutaka kusababisha vurugu na machafuko nchini Korea kusini, kwa kujaribu kutangaza matumizi ya sheria ya kijeshi mwezi Desemba.
Mahakama mjini Seoul imetoa hati ya kukamatwa leo Jumanne, na kumfanya Yoon kuwa rais wa kwanza wa Korea kusini, aliye madarakani, kutakiwa akamatwe.
Bunge lilipiga kura ya kumuondoa madarakani Yoon kati kati mwa mwezi Desemba, na kuondoa nguvu zake za rais wakati mahakama ya kikatiba ina thathmini kesi dhidi yake.
Yoon vile vile anachunguzwa kwa kujaribu kusababisha vurugu na matumizi mabaya ya Madaraka.
Alikaidi agizo mara tatu, kutaka kufika mbele ya maafisa wa uchunguzi, hatua ambayo imepelekea mahakama kutoa amri ya kutaka akamatwe.
Mawakili wake wametaja hatua hiyo kuwa kinyume cha sheria na kwamba watawasilisha kesi mahakamani kupinga uamuzi huo.
Forum