Waasi wanaoungwa mkono na Rwanda waliteka sehemu kubwa za mji mkubwa wa mashariki mwa Congo ukiwemo uwanja wake wa ndege, Umoja wa Mataifa ulisema, wakati rais wa Rwanda siku ya Jumatano alijiunga na wito wa kusitishwa mapigano katika mzozo huo wa miongo kadhaa.
Sehemu kubwa ya mji uliokumbwa na mzozo wa Goma zilikuwa shwari mapema Jumatano asubuhi, baada ya siku ambayo maelfu ya watu waliokuwa wakikimbia walijificha kando ya barabara huku makombora yakirushwa na kujeruhi watu ambao walimiminika kwenye hospitali zilizoelemewa na wagonjwa.
Wakati vikosi vya serikali bado vinadhibiti baadhi ya sehemu za Goma, wakazi waliozungumza na shirika la habari la Associated Press kwa njia ya simu siku ya Jumanne walisema kuwa waasi wa M23 wanadhibiti sehemu kubwa ya mji huo.
Rais wa Rwanda Paul Kagame alisema kwenye mtandao wa X kwamba alizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio juu ya haja ya kuhakikisha sitisho la mapigano na kushughulikia sababu za msingi za mzozo huo mara moja na kwa ukamilifu.
Forum