Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 09, 2025 Local time: 06:16

Marekani yasema RSF imefanya mauaji ya kimbari Sudan


Kiongozi wa RSF Mohamed Daglo. (Photo by ASHRAF SHAZLY / AFP)
Kiongozi wa RSF Mohamed Daglo. (Photo by ASHRAF SHAZLY / AFP)

Utawala wa Rais wa Marekani Joe Biden Jumanne umesema kuwa kundi la kijeshi la Sudan la Rapid Support Forces, RSF, pamoja na washirika wake wanatekeleza mauaji ya kimbari.

Kundi hilo limekuwa kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe na jeshi la serikali ambavyo vimeua maelfu ya watu, na kwa hivyo kuongeza vikwazo kwa kiongozi wake pamoja na makampuni shirika.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken amesema kuwa ghasia hizo zilizoanza karibu miaka miwili iliyopita na ambazo zimesababisha janga baya zaidi la kibinadamu duniani, ni zaidi ya uhalifu wa kivita na maangamizi ya kikabila, wakati wa hotuba yake ya Desemba mwaka jana.

Blinken alisema kuwa kutokana na ripoti za karibuni, aligundua kuwa kundi la RSF, linafanya mauaji ya halaiki. “RSF na washirika wake wameendelea kufanya mashambulizi ya moja kwa moja dhidi ya raia."Alisema Blinken. UAE ambao ni muungano wa falme 7 kwenye Peninsula ya Kiarabu na mshirika wa karibu wa Marekani umekuwa ukishutumiwa kwa kutoa silaha kwa RSF, dai ambalo limeendelea kukanusha vikali.

Vita kati ya RSF na vikosi vya serikali ya Sudan vilizuka Aprili 2023, vikiripotiwa kusababisha zaidi ya vifo 28,000 na kulazimisha mamilioni ya watu kutoroka makwao. Baadhi yao wameripotiwa kula nyasi kutokana na uhaba mkubwa wa chakula uliosababishwa na ukame.

Forum

XS
SM
MD
LG