Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 07, 2025 Local time: 03:06

Rais Trump ametia saini amri kadhaa za kiutendaji ikiwemo uhamiaji


Rais wa Marekani Donald Trump akiweka saini moja ya amri kadhaa za kiutendaji katika muhula wake wa pili madarakani. January 20, 2025. (Photo by Jim WATSON / POOL / AFP)
Rais wa Marekani Donald Trump akiweka saini moja ya amri kadhaa za kiutendaji katika muhula wake wa pili madarakani. January 20, 2025. (Photo by Jim WATSON / POOL / AFP)

Miongoni mwa amri za kiutendaji zililenga uhamiaji kama vile kutangaza hali ya dharura kwenye mpaka wa Marekani na Mexico.

Rais wa Marekani Donald Trump amechukua hatua kadhaa za kiutendaji baada ya kuingia madarakani Jumatatu, ikijumuisha kujiondoa katika mashirika ya afya ya kimataifa na mkataba wa hali ya hewa wa Paris, na ameelekeza kusimamishwa kwa muda misaada ya kigeni ya Marekani.

Amri kadhaa zililenga uhamiaji, kama vile kutangaza hali ya dharura kwenye mpaka wa Marekani na Mexico, kusitisha kuomba hifadhi na kusitisha haki ya uraia wa kuzaliwa kwa watoto waliozaliwa nchini Marekani.

Trump pia aliamuru ufanyike uchunguzi kwa kiwango cha juu iwezekanavyo kwa watu wote wanaotaka kuingia Marekani, na kwa serikali kuzitaja nchi ambazo zina matatizo ya uchunguzi ili kuwazuia raia wake kuingia nchini Marekani.

Katika muhula wake wa kwanza madarakani, Trump alifuata sera ya kigeni ya Marekani Kwanza, na amri aliyoisaini Jumatatu inamuelekeza Waziri mpya wa Mambo ya Nje Marco Rubio kulenga juhudi za wizara ya mambo ya nje kwa ujumbe huo.

Forum

XS
SM
MD
LG