Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 17, 2025 Local time: 02:45

Mpinzani Kiiza Besigye wa Uganda ameongezewa mashtaka ya usaliti


Kiiza besigye, kiongozi wa upinzani nchini Uganda.
Kiiza besigye, kiongozi wa upinzani nchini Uganda.

Amekuwa kizuizini katika mji mkuu wa Kampala tangu alipokamatwa Novemba 2024 akiwa na msaidizi Obeid Lutale.

Waendesha mashtaka wa jeshi la Uganda leo Jumatatu waliongeza mashtaka ya usaliti ambayo yanapewa adhabu ya kifo kwenye orodha ya ukiukwaji wa sheria za kijeshi ambapo wanasema ulifanywa na kiongozi huyo maarufu wa upinzani.

Kiiza Besigye hasimu mkongwe wa kisiasa wa Rais Yoweri Museveni, ambaye yupo madarakani kwa karibu miaka 40 alikamatwa katika nchi jirani ya Kenya mwezi Novemba.

Alirudishwa nyumbani Kampala na kushtakiwa kwa kumiliki silaha kinyume cha sheria na alisomewa mashtaka katika mahakama ya jeshi kwa kuhujumu usalama wa nchi hiyo ya Afrika Mashariki, licha ya kuwa raia.

Amekuwa kizuizini katika mji mkuu wa Kampala tangu wakati huo. Akiwa pamoja na msaidizi Obeid Lutale ambaye naye alikamatwa na kushtakiwa.

Mke wa Besigye, Winnie Byanyima ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa UNAIDS anasema kuwa mashtaka dhidi ya Besigye ni ya kisiasa. Mawakili wake wanakanusha mashtaka hayo kuwa hayana msingi.

Wakati wa usikilizaji kesi leo Jumatatu mwendesha mashtaka wa kijeshi alimsomea Besigye na mwenzake mashtaka mapya ya usaliti.

Kulingana na karatasi ya mashtaka iliyoonekana na shirika la Habari la Reuters, Besigye na mtuhumiwa mwenza walipanga ujasusi kuhusu njama ya kudhoofisha usalama wa taifa, lakini walilazimika kuzuia hatua hiyo ilisema taarifa kutoka kwa mamlaka husika.

Mawakili wa Besigye walipinga mashtaka hayo ya ziada, wakisema kuwa yalikiuka taratibu za kesi za jinai.

Forum

XS
SM
MD
LG