Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Januari 21, 2025 Local time: 13:42

Wanajeshi watano wa Cameroon wauawa na watu wenye silaha kutoka Nigeria


Ramani ya mpaka kati ya Cameroon, Chad na Nigeria
Ramani ya mpaka kati ya Cameroon, Chad na Nigeria

Watu wenye silaha kutoka Nigeria wamewaua wanajeshi watano wa Cameroon na kuwajeruhi wengine kadhaa katika kijiji cha Bakinjaw kwenye mpaka wa Cameroon na Nigeria, mbunge wa wilaya alisema Jumamosi.

Aka Martin Tyoga, mbunge wa wilaya ya Akwaya kusini magharibi mwa Cameroon, ambako mauaji hayo yalitokea, aliiambia Reuters kwamba shambulizi hilo lilifanyika mapema Ijumaa, wakati mamia ya wafugaji wenye silaha kutoka jamii ya Fulani walivuka mpaka kutoka jimbo la Taraba nchini Nigeria kushambulia kituo cha kijeshi.

Amesema shambulizi hilo ilikuwa ulipizaji kisasi baada ya wanajeshi wa Cameroon kuwaua wafugaji kadhaa siku moja kabla.

Forum

XS
SM
MD
LG