Fawzia Amin Saydo mwenye umri wa miaka 21 alitekwa nyara na wanamgambo wa Islamic State kutoka kwenye mji wake wa nyumbani wa Sinjar, kaskazini mwa Iraq, Agosti 2014, mwezi mmoja kabla ya kusherehekea siku kuu ya kuzaliwa ya miaka 11.
Baada ya hapo alipitia maisha ya mateso kwa muongo mmoja, huku akibakwa, kuzuilia na kulazimishwa ndoa kwa mpiganaji wa ISIS nchini Syria kabla ya kupelekwa Gaza ili kuishi na mama wa mtekaji wake. Hatimaye aliokolewa Gaza hapo Oktoba 1, 2024 kwenye operesheni ya Marekani iliyojumuisha wanaharakati wa haki za binadamu pamoja na maafisa wa Israel, Jordan, Iraq na Umoja wa Mataifa.
Sydo aliwasili kwenye uwanja wa ndege wa Hannover wa Ujerumani Jumanne saa 11 jioni ambapo alipokelewa na wakili wake, Kareba Hagemann, wanafamilia kadhaa pamoja na wanaharakati wa haki za binadamu. “Amewasili Ujerumani salama na amefurahi sana,” Hagemann aliambia VOA. Ubalozi wa Ujerumani mjini Baghdad Februari 10 ulipatia Saydo visa ya kusafiria kwa misingi ya kibinadamu. Kwa mujibu wa shirika la wakambizi la Umoja wa Mataifa, Ujerumani ni taifa la tatu linalotoa hifadhi kwa wakimbizi wengi zaidi ndani ya Umoja wa Ulaya.
Forum