China ililalamikia ushuru uliyotangazwa na rais wa Marekani Donald Trump kwenye kikao cha WTO Jumanne, wakati Washington ikipuzia matamshi ya China kuwa ya kinafik. Trump alitangaza ushuru wa asilimia 10 kwenye bidhaa kutoka China, na kupelekea Beijing kujibu kwa kuwekea Marekani ushuru pamoja na kushtaki Washington kwa WTO, hatua inayoonekana kama kipimo cha namna Trump anavyoichukulia taasisi hiyo.
Mengi ya mataifa 6 yaliyoshiriki mazunguzo hayo na kujadili malalamishi ya China yalieleza wasi wasi kutokana na taharuki za kibiashara, msemaji wa WTO, Ismalia Deing aliambia wanahabari Jumatano akiwa mjini Geneva, Uswizi. Baadhi ya mataifa yaliyoshiriki mazungumzo hayo ni pamoja na Marekani, Nicaragua, Namibia, Malaysia, Trinidad na Tobago na Russia ikiwa sehemu ya mazungumzo pana kuhusu biashara ya kimataifa.
Vyanzo viwili vya kibiashara vilivyoshiriki mazungumzo hayo viliambia shirika la habari la Reuters kwamba wengi wa waliyoshiriki walielezea wasi wasi wao kuhtokana na kuongezwa kwa ushuru.
Forum