Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 02, 2025 Local time: 20:28

Marekani yaongeza maradufu wafungwa wa Guantanamo Bay


Jela ya Guantanamo Bay, Cuba, Feb. 6, 2025.
Jela ya Guantanamo Bay, Cuba, Feb. 6, 2025.

Marekani imeongeza maradufu idadi ya wafungwa wanaodhaniwa kuwa tishio kubwa pamoja na wale wanaosubiri kurejeshwa makao kwenye kituo cha jeshi la wanamajaji la Marekani cha Guantanamo Bay nchini Cuba.

Kufikia Jumanne kulikuwa na zaidi watu 120 ambao serikali imetaja kuwa wahalifu, wakiwa chini ya uangalizi, maafisa wa ulinzi wa Marekani wamesema. Takriban watu wengine 50 wanashikiliwa kwenye sehemu maalum ya wahamiaji ambayo inaandaliwa kwa ajili ya kushikilia watu wasio na fujo.

Kwenye taarifa nyingine afisa wa ulinzi wa Marekani ameambia VOA kwamba kufikia Jumatatu, jeshi la Marekani lilikuwa limepeleka ndege 13 za wahamiaji wasiyo na stakabadhi huko Guantanamo Bay. Maafisa waliyozungumza na VOA hawakutaka kutambulishwa kwa kuwa uperesheni za kijeshi ni nyeti.

VOA pia imejaribu kufikia Wizara ya Usalama wa Ndani inayoongoza operesheni ya kuondoa wahamiaji nchini, pamoja na Idara ya Uhamiaji kuhusu ongezeko kubwa la watu waliyoshikiliwa. Afisa mmoja akizungumza na VOA bila kutaka kutajwa amesema kuwa watu wote wanaoshikiliwa Guantanamo tayari wamepewa stakabadhi za mwisho za kurejeshwa makwao.

Forum

XS
SM
MD
LG