Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 02, 2025 Local time: 18:51

Pentagon kupendekeza kupunguza matumizi ya fedha


Jengo la Pentagon lililopo Arlington, Virginia, Marekani.
Jengo la Pentagon lililopo Arlington, Virginia, Marekani.

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Pete Hegseth ameomba baadhi ya vitengo vya jeshi kupendekeza matumizi yatakayo punguzwa kama sehemu ya punguzo la asilimia 8 ndani ya kila mwaka kwa miaka 5 mitano ijayo.

Hayo yamesemwa na maafisa wa Marekani Jumatano, ingawa haijabainika iwapo bajeti yote ya ulinzi itapunguzwa. Kwenye waraka uliyooneshwa shirika la habari la AP na maafisa wa Marekani, Hegseth alitaka mapendekezo hayo yafanyike kufikia Februari 24. Maafisa wamesema kuwa Hegseth halengi punguzo kubwa la bajeti lakini analenga kulainisha vipaombele kuendana na azma ya Rais wa Marekani Donald Trump kuhusu usalama wa taifa.

Bajeti ya Pentagon inakaribia dola trilioni kwa mwaka. Desemba mwaka jana Rais Joe Biden alitia saini msuada wa kuidhinisha dola bilioni 895 kwenye ulinzi kwa mwaka wa kifedha unaomalizika Septemba 30. Hegseth amesema hadharani kwamba lengo la Pentagon ni kuimarisha usalama wa mipaka pamoja na tishio la China.

Amesema kuwa Marekani haiwezi kuendelea kuzingatia usalama wa Ulaya. Hali ya wasi wasi imetanda miongoni mwa wafanyakazi wa Pentagon, baada ya timu ya mfanyabiashara Elon Musk kuanza kutadhimini shughuli za Pentagon.

Forum

XS
SM
MD
LG