Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 02, 2025 Local time: 15:57

Hamas wamewachilia miili ya mateka 4


Wanamgambo wa Hamas wameachilia miili ya mateka waliouawa, Khan Younis. Februari 20 2025. PICHA: Reuters
Wanamgambo wa Hamas wameachilia miili ya mateka waliouawa, Khan Younis. Februari 20 2025. PICHA: Reuters

Wanamgambo wa Hamas wameachilia miili ya waisrael wanne, na kusafirishwa kwa msafara wa magari ya shirika la msalaba mwekundu kutoka Khan Younis, kusini mwa Gaza.

Mamia ya watu wamekusanyika kwa ajili ya kupokea miili hiyo katika sehemu ambayo wapiganaji waliwasilisha miili hiyo ikiwa kwenye majeneza ya rangi nyeusi, na yaliyofunikwa kwa bendera na kuwekelewa mabango.

Mojawapo ya mabango hayo yalimshutumu Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kwa kuwa mhalifu wa kivita na kwamba kudai mashambulizi ya Israel ndiyo yaliyowaua mateka.

Ofisi ya Netanyahu imesema kwamba shirika la msalaba mwekundu lilipeleka mabaki ya waliouawa kwenye kambi ya jeshi ya Israel na kwamba yatafanyiwa uchunguzi kwenye kituo cha kitaifa cha tiba mjini Tel Aviv ili kuwatambua waliofariki.

Miongoni mwa mateka waliowachiliwa leo Alhamisi ni mtoto mwenye umri mdogo kabisa Kfir Bibas, aliyekuwa na umri wa miezi tisa alipotekwa nyara na wanamgambo hao, Pamoja na ndugu yake mwenye umri wa miaka 4 Ariel Bibas na mama yao Shiri Bibas.

Walitekwa nyara na Hamas Oktoba 7 2023.

Forum

XS
SM
MD
LG