Miongoni mwa miradi hiyo ni ule wa bomba la mafuta la Enbridge Line 5, chini ya ziwa Michigan, vinu kadhaa vya gesi asilia pamoja na vituo vya upelekaji gesi vilivyo pendekezwa na makampuni ya Cheniere na Venture Global.
Trump kwenye amri ya kiutendaji siku ya kwanza baada ya kuapishwa aliamuru wahandisi hao kutoa vibali vya kutumika kwa maeneo yenye maji pamoja kuchimbwa au kutengenezwa kwa njia za maji kama sehemu ya Dharura ya Kitaifa ya Nishati.
Hata hivyo kuharakishwa kwa miradi hiyo huenda kukazua mivutano ya kisheria kutokana na vibali vingi vinavyohitajika, wakati makundi ya kulinda mazingira yakionya kuwa ni ukiukwaji wa sheria za serikali kuu. Makampuni yenye kandarasi ambazo zinasubiri vibali yamekaribisha pendekezo hilo.
Forum