China imekuwa ikilengwa sana na rais Trump katika sera yake ya nyongeza ya ushuru.
Trump ameambia waandishi wa habari kwamba China ilikuwa tayari imefikia makubaliano na Marekani kuhusu kile ametaja kama makubaliano mazuri sana ya kibiashara na China mnamo mwaka 2020, akiongezea kwamba makubaliano mapya yanaweza kupatikana.
Wizara ya mambo ya Nje wa China imesema leo Alhamisi kwamba nchi hizo mbili zinastahili kushughulikia mgogoro wao wa kibiashara kwa kuzingatia heshima kutoka pande zote mbili.
Trump ametishia kuwekea ushuru wa ziada washirika wa Marekani Pamoja na wasiokuwa washirika, akiwa amemaliza mwezi mmoja ofisini.
Nyongeza ya ushuru imelenga China, Canada, Mexico na umoja wa Ulaya.
Forum