Gavana wa Odesa Oleh Kiper ameandika ujumbe kwente Telegram kwamba wafanyakazi wanaendelea na juhudi za kurudisha umeme.
Nyumba 49,000 zilikuwa hazina umeme kufikia wakati tunaandaa ripoti hii.
Mashambulizi ya Russia yameendelea leo Alhamisi katika sehemu kadhaa za Ukraine ikiwemo katika eneo la Katikati la Cherkasy ambapo gavana Ihor Taburets amesema mfumo wa ulinzi wa angani umeangusha ndege 14 zisizokuwa na rubani, za Russia.
Taburets amesema kwamba uharibifu umetokea kwenye biashara na kukatiza nguvu za umeme lakini hakuna vifo vimeripotiwa.
Gavana wa Mykolaiv Vitaliy Kim, ameripoti kwamba jeshi limeangusha ndege isiyokuwa na rubani iliyokuwa inapaa eneo hilo.
Wizara ya ulinzi ya Russia imesema imeharibu ndege nne zisizokuwa na rubani za Ukraine, usiku wa kuamkia leo, ikiwemo katika eneo linalokaliwa na Russia la Crimea na Bryansk.
Forum