Lebanon ilizuia ndege ya Iran kuingia Beirut siku ya Alhamisi baada ya Israel kuishutumu Iran siku moja kabla kwa kutumia ndege za kiraia kupeleka fedha kwa kundi la kigaidi la Hezbollah nchini Lebanon.
Afisa mkuu mtendaji wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Imam Khomeini, Saeed Chalandri ameliambia shirika la habari la Iran, la Mehr kwamba safari ya ndege ya Mahan Air kuelekea Beirut ilifutwa kabla ya kupaa kwa sababu Lebanon haikutoa ruhusa ya kutua.
Katika video iliyowekwa kwenye mtandao wa X na mwandishi wa habari anayeishi Iran na kuonekana kuwa taarifa za kuaminika na VOA Idhaa ya Persian, abiria hao walionekana wakisubiri katika ukumbi wa abiria kuondoka uliotengwa kwa ajili ya mahujaji wa kidini huku mtu mmoja akipiga kelele akielezea kusikitishwa kutokana na hatua ya kukwama hapo.
Forum