Maoni hayo yametolewa wakati mawaziri wa ulinzi wa NATO walipokusanyika mjini Brussels, Ubelgiji, kwa mkutano uliolenga suala la bajeti za ulinzi, kuongeza uwezo wa kiviwanda na uungwaji mkono kwa Ukraine.
Mkutano huo unafanyika huku kukiwa na msukumo kutoka Marekani kwa washirika wa NATO kuongeza bajeti zao za katika ulinzi, wakati ambapo Rais wa Marekani Donald Trump ameashiria kuwa hivi karibuni atafanya mazungumzo na Rais wa Russia Vladimir Putin.
"Hakuwezi kuwa na mazungumzo kuhusu Ukraine bila Ukraine. Na sauti ya Ukraine lazima iwe msingi wa mazungumzo yoyote," Waziri wa Ulinzi wa Uingereza John Healey aliwaambia waandishi wa habari kabla ya mkutano huo wa mawaziri.
Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Boris Pistorius alisema uwezekano wa Ukraine kuwa mwanachama katika NATO na iwapo inapaswa kukubali eneo lolote litwaliwe, haupaswi kuamuliwa kabla ya mazungumzo ya amani kuanza.
Forum