Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 02, 2025 Local time: 17:04

Ukraine imeahidiwa msaada zaidi wa silaha


Katibu mkuu wa NATO General Mark Rutte akihutubia mkutano wa muungano huo, Brussels. February 12, 2025.
Katibu mkuu wa NATO General Mark Rutte akihutubia mkutano wa muungano huo, Brussels. February 12, 2025.

Waziri wa ulinzi wa Ukraine Rustem Umerov, amesema kwamba mkutano wa washirika wa nchi hiyo, unaofanyika Brussels leo Jumatano, unaangazia namna ya kutoa silaha zaidi kwa Ukraine, ikiwemo mifumo muhimu ya ulinzi.

Matamshi ya Umerov yanajiri kabla ya mkutano huo wa ulinzi unaozileta Pamoja nchi 50 ambazo zimekuwa zikisaidia Ukraine tangu uvamizi wa Russia ulipoanza mwaka 2022.

Umerov amesema kwamba mazungumzo yataangazia pia uekezaji katika sekta ya ulinzi ya Ukraine na ushirikiano katika miradi mbalimbali na washirika wake wa Ulaya.

Waziri wa ulinzu wa Uingereza John Healey anaongoza mkutano huo kwa mara ya kwanza ambao ulikuwa ukiongozwa na Waziri wa ulinzi wa Marekani.

Healey amesema wataongeza msaada kwa Ukraine, kuongeza ulinzi kupitia kwa NATO na kupata amani kupitia ushirikiano.

Waziri mpya wa ulinzi wa Marekani Pete Hegseth anatarajiwa kuhutubia mkutano katika makao makuu ya NATO, siku moja kabla ya mawaziri wa ulinzi kutoka nchi wanachama wa NATO kukutana.

Forum

XS
SM
MD
LG