Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 03, 2025 Local time: 00:00

Belarus yamwachilia mwanahabari wa radio inayofadhiliwa na Marekani


Mwandishi wa habari wa Radio Free Europe/Radio Liberty, Andrey Kuznechyk
Mwandishi wa habari wa Radio Free Europe/Radio Liberty, Andrey Kuznechyk

Mwandishi wa habari wa chombo cha habari dada cha VOA, Radio Free Europe/Radio Liberty, aliachiliwa kutoka Belarus Jumatano baada ya kufungwa jela kwa zaidi ya miaka mitatu. Kesi yake ilionwa na wengi kama iliyochochewa kisiasa.

Andrey Kuznechyk wa Radio Free Europe/Radio Liberty, idhaa ya Belarus, aliachiliwa pamoja na watu wengine wawili, alisema mjumbe maalum wa Marekani anayehusika na masuala ya mateka Adam Boehler, ambaye hakufafanua utambulisho wa mateka hao wengine wawili.

Rais wa Radio Free Europe/Radio Liberty Stephen Capus amefurahiswa na kuachiliwa kwa Kuznechyk na kumshukuru Rais Donald Trump, waziri wa mambo ya nje Marco Rubio na serikali ya Lithuania kwa mchango wao ili mwandishi huyo wa habari aachiwe huru.

“Hii ni siku ya furaha kwa Andrey, mke wake, na watoto wao wawili. Baada ya kutengana kwa zaidi ya miaka mitatu,

Forum

XS
SM
MD
LG