Jaji wa tatu wa serikali kuu ya Marekani leo Jumatatu alizuia amri ya Rais Donald Trump ya kusitisha uraia wa kuzaliwa kwa watoto wa watu ambao wako Marekani kinyume cha sheria.
Uamuzi huo wa jaji Joseph N. Laplante katika jimbo la New Hampshire umekuja baada ya hukumu mbili kama hizo kutolewa na majaji katika majimbo ya Washington State na Maryland wiki iliyopita. Kesi iliyowasilishwa na American Civil Liberties Union inasema kuwa amri ya Trump inakiuka Katiba na inajaribu kuimarisha moja ya maadili ya msingi ya kikatiba ya Marekani. Utawala wa Trump wa Republican umedai kuwa watoto wanaozaliwa na watu wasio raia hawako chini ya mamlaka ya Marekani na kwa hivyo hawana haki ya uraia.
Utawala huo unakata rufaa dhidi ya uamuzi wa jaji wa mji wa Seattle katika jimbo la Washington State kuhusu amri ya Trump. Kiini cha mashtaka hayo kwenye kesi tatu ni Marekebisho ya 14 ya Katiba yaliyoidhinishwa mnamo mwaka 1868 baada ya Vita vya wenyewe kwa wenyewe na uamuzi wa Mahakama ya juu ya Dred Scott ambayo ilishikilia kwamba Scott, mwanamme mtumwa hakuwa raia licha ya kuishi katika hali ambayo utumwa ulipigwa marufuku.
Mwaka 1898 katika kesi inayojulikana kama Marekani dhidi ya Wong Kim Ark, Mahakama Kuu ya Marekani iligundua watoto pekee ambao hawakupata uraia wa Marekani moja kwa moja baada ya kuzaliwa kwenye ardhi ya Marekani walikuwa watoto wa wanadiplomasia ambao wanatii kwa serikali nyingine, maadui waliopo Marekani wakati wa uvamizi wa uhasama wale waliozaliwa kwenye meli za kigeni na wale waliozaliwa na wanachama wa makabila huru yenye asili ya Marekani.
Forum