Kiwanda cha kusafisha mafuta cha Dangote nchini Nigeria ambacho ni kikubwa zaidi barani Afrika kinaweza kuanza kufanya kazi kwa ukamilifu ndani ya siku 30 mkuu wa kiwanda hicho alisema Jumatatu.
Kikiwa na uwezo wa kuzalisha mapipa 650,000 kwa siku kiwanda hicho kilijengwa na bilionea wa Nigeria Aliko Dangote mjini Lagos kilianza kusafisha mafuta ghafi hadi bidhaa ikijumuisha dizeli pamoja na mafuta ya ndege hapo mwezi Januari mwaka jana na kilianza kuzalisha petroli mwezi Septemba.
Kinalenga kushindana na wazalishaji mafuta wa Ulaya wakati kinapoanza kufanya kazi kamili lakini kilikuwa kinataabika kupata mafuta ghafi ya kutosha ya ndani. Edwin Devakumar mkuu wa kiwanda cha kusafisha mafuta cha Dangote alisema kuwa kiwanda hicho kilikuwa kinafanya kazi kwa uwezo wa asilimia 85 na tunaweza kwenda asilimia 100 katika kipindi cha siku 30.
Mwaka jana kiwanda hiki kilibadilika na kuanza kuagiza kutoka nje mafuta ghafi baada ya kutokuweza kupata kiasi cha kutosha licha ya makubaliano ya serikali ya Nigeria kununua mafuta ghafi kwa kutumia sarafu ya ndani ya Naira.
Forum