Tangazo hilo limekuja muda mfupi baada ya kuchukua hatua sawa kwa washirika watatu wakubwa wa kibiashara wa Marekani- Canada, Mexico na China. Starmer aliyasema hayo wakati akiwa mwenyeji wa Chansela wa Ujerumani Olaf Scholz kwenye makao yake ya mashambani wakati wakizungumzia kuimarishwa kwa ushirikiano na Umoja wa Ulaya.
Canada na Mexico waliwekea Marekani ushuru wa ziada, kama majibu, baada ya Trump Jumanne kutangaza ushuru wa asilimia 25 dhidi ya mataifa hayo, huku China ikiwekewa asilimia 10 dhidi ya bidhaa zake zinaoingia Marekani. Trump alisema kuwa kwa hakika anapanga kuongeza ushuru kwa mataifa ya EU.
Uingereza ilijiondoa kwenye EU, 2020, kufuatia kura ya maoni ya 2016. Trump ambaye alikuwa muungaji mkono mkubwa wa kujiondoa kwa Uingereza kwenye EU kupitia kura ya Brexit bado hajasema iwapo anapanga kuwekea Uingereza ushuru wa ziada.
Hatua hiyo ya Marekani imezua wasi wasi wa kutokea kwa vita vya kibiashara vya kimataifa. Starmer Jumatatu anaelekea Ubelgiji ili kukutana na viongozi wa EU, akilenga kutadhmini upya uhusiano wa taifa lake na muunguno huo.
Forum