Serikali ya China pia imetishia kupitisha hatua za kukabiliana na baadhi ya wafanyabiashara wa China wakielezea wasiwasi wao kuhusu uwezekano wa kuvurugika kwa mauzo yao ya nje kwenye soko la Marekani.
Wakati Wizara ya Biashara ya China ikiapa kupinga hatua ya utawala wa Rais Trump katika Shirika la Biashara Duniani, wizara ya mambo ya nje ya China imesisitiza kwamba vita vya biashara na ushuru haviwezi kutatua matatizo ya Marekani nyumbani na muhimu zaidi, havina manufaa kwa upande wowote.
Awali Rais Trump alisema ushuru wa ziada kwa bidhaa za China ni jibu la Washington kwa jukumu la China katika utengenezaji wa kemikali za awali muhimu kwa uzalishaji wa fentanyl, nchini Mexico.
Forum