Rubio ameambia rais wa Panama Jose Raul Mulino na waziri wa mambo ya kigeni Javier Martinez Acha, wakiwa kwenye mji wa Panama City, kwamba Rais wa Marekani Donald Trump amefanya maamuzi ya kwanza kwamba msimamo wa sasa, ushawishi na udhibiti wa Chama cha Kikomumisti cha China kwenye mfereji wa Panamana ni tishio kwenye operesheni zake, wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema.
Hata hivyo taarifa hiyo haikufafanua ni ushawishi wa aina gani ambao Marekani inadai kuwa nao kwenye mfereji huo wenye urefu wa kilomita 82 kati ya bahari za Atlantic na Pacific, hatua inazopanga kuchukua, wala majibu ya Rais wa Panama kutokana na taarifa ya Rubio. Rais huyo katika siku za karibuni amelalamikia ukosoaji kutoka Marekani hukusu namna mfereji huo unavyoendeshwa, ukiwa na umuhimu mkubwa kwenye biashara za kimataifa.
Hata hivyo alisema kuwa hakutakiwa na majadiliano yoyote na Marekani kuhusu umiliki wa mfereji huo, huku baadhi ya wakazi wa Panama wakifanya maandamano kupinga mpango wa Marekani.
Forum