Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 31, 2025 Local time: 03:17

RSF yaunda serekali na washirika wake Nairobi


Picha ya Maktaba
Picha ya Maktaba

Vikosi vya akiba vya Sudan (RSF) na washirika wake Jumapili wamekubaliana kuunda serikali ya pamoja, licha ya onyo kwamba hatua hiyo inaweza kuisambaratisha zaidi nchi hiyo iliyoharibiwa na vita.

Pande za makubaliano hayo, zilitia saini katika mkutano wa faragha Nairobi, Kenya, na kusema mkataba huo unaanzisha serikali ya amani na umoja katika maeneo yanayodhibitiwa na waasi katika nchi hiyo ya kaskazini mashariki mwa Afrika.

Hatua hiyo imefanyika baada ya takriban miaka miwili ya vita mbaya na jeshi la Sudan, ambayo imesumbua watu zaidi ya milioni 12 na kusababisha kile Umoja wa Mataifa unakiita njaa kubwa zaidi na migogoro ya watu kuyahama makazi yao.

Wakati huohuo, waziri wa mambo ya nje wa serikali ya kijeshi ya Sudan, Ali Yousseff, Jumapili akiwa Cairo, Misri amesema Sudan haitakubali na kuitambua serekali hiyo ya muungano chini ya RSF, pamoja na nchi yoyote itakayo itambua.

Forum

XS
SM
MD
LG